spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers
spacers home the model find a video Product spacer
spacer Help search Sitemap about
line

Misingi ya Demokrasia

 

    

Ufupisho

Kama mtu aliyeelimika, mwanafunzi anahitajika kuwa na mbinu za mawasiliano (uwezo wa kuongea, kusikiliza, kusoma, kuandika, na kutafakari kwa makini), mbinu makinifu, (uwezo wa kutambua na kuelewa fikra za wenzake, na mahusiano katika mandendo mabalimabali, uelevu, na thamini), na mbinu za kuishi kidomokrasia. Hizi zinahusisha, uvumilivu, umakinifu, kufikiri pamoja na kufanya maana, kugawana madarak na uwezeshaji, uwajibikaji wa binafsi na kujihusisha kiraia na wengine. Hizi maada za demokrasia zitawawezesha wengine kuwaandaa wanafunzi kuwa na maisha mazuri yanayoendana na misingi ya demokrasia.

Demokrasia ya baadaye inategemea jinsi tunavyofanikiwa sasa. Wakati mwingine watu wanajaribu kutenganisha misingi hiyo kulingana najinsi wanavyojihusisha na kila kipengele cha misingi hiyo. Watu (na hasa vijana) wanatakiwa wasaidie kujitambua wenyewe kwa uhakika na kutambua kikundi chao na kuheshimu wenzao kwa jinsi walivyo. Kama watu wamewekwa ana kwa ana na matukio kinyume cha matakwa ya kujipenda na chuki, watatakiwa kuangalia na kuyatathmini maisha yao wenyewe. Kuelewa ni jinsi gani hii inaweza kutokea, inabidi kwanza kuelewa uvumilivu.

Kunzia na uvumilivi,  uwezo wa au mazoezi ya kutambua  na kuheshimu imani na maisha yaw engine (The American Heritage Dictionary, 1982) au  “huruma na kujitolea kwa imani na matendo yanayotofautiana kati yako na wengine na kitendo ya kuruhusu kitu fulani (Webster, 1991).  Tunahitaji kuelewa zaidi jinsi watu wanavyojifunza kuwavumilia wale wanaowafikiria ni tofauti nao.  Wanafunzi wanahitaji kujiamini wenyewe na wenzao kwa pamoja kuheshimu na kukubali tofauti kati yao na wenzao.

Kuwa mvumilivu, unahitajiwa kufuata hatua nyingi:

  • Kujifunza kuwa wengine wanatokea katika mazingira gain kwa kuwauliza wenzao wawaeleze hadithi zao

  • Kusikiliza bila kujaji
  • Kuuliza maswali ili kuthibitisha uelewa wao, kulinganisha imani yao na imani za wengine
  • Kuainisha mafanano na tofauti katika mifumo ya imani
  • Kutathmini tofauti hizi
  • Kuainisha kupitia kuulizia na kujua kama imani hizi au zingine zinaweza kubadilika
  • Kujaribu uhaki na sheria zinalinda hizo imani katika pande zote mbili.

Kama pande zote ni halali kotokana na mila na pande zote zinaruhusu mabadiliko, wewe na mwngine yeyote yaweza kuamua kuwa wavumilivu kati yao (Fisher & Brown, 1988).  Inakuwaje kama mmoja ataamua kutokufanya hili; basi kwanini ya mafikirio yao yanatakiwa yaangaliwe kwa makini na hii inaweza ikafanikishwa kutokana na umakinifu wa mafikirio.  Inavyokubalika kuwa ni lengo muhimu katika elimu umakinifu wa kufikiria na inafanannishwa na lengo la kama utambuzi, kujitawala, na labda kipaji cha kubuni na akili.  Watu wanaofikiria kwa umakinifu huendelea kwa misingi ya kutathmini kwa makini, bila upendeleo, vitu wanavyoviona na kuweza kufikia maamuzi ya hakika kabisa kwa kufikiria vigezo vinavyofaa na  mantiki yenye sababu na njia thabiti (Good, 1973)

Siege (kama ilivyonukuriwa na Husen & Psotlethwaite, 1994, 1206 – 1207) wanashauri uthibitisho wa fikra za umakinifu ya elimu katika masharti yafuatayo:

  1. mfano bora wa kuheshimu wengine unahitaji kuheshimu haki za wanafunzi kuuliza maswali, kutafuta sababu, maelezo, na uthibitisho;

  2.  umakinifu wa fikra ni lazima kuendeleza maamuzi huru ya mwanafufuzi yanayohitajika kwa mwanafunzi kujitosheleza atakapokuwa mtu mzima.

  3. Umakinifu wa fikra huleta haya yaliyoelezwa hapoawali (a. & b. ) maelekeo, mtazamo, na nyenzo na;

  4. Umakinifu wa fikra ni kitovo cha aina ya maamuzi ya akili yanayohitajiwa na raia katika demokrasia.

Kwa hiyo umakinifu wa fikra inaundwa na uchunguzi mantiki.

Ufanyaji maamuzi katika demokrasia ni njia ya kufikia makubaliano katika mazingira ya kikundi kupitia mazungumzo, majadiliano, mdahalo, na uchanganuzi.  Katika jamii wazi na yenye nguvu raia wan bahati ya kutoa maamuzi katika serikali yao.  JAmii katika demokrasia hufanya maamuzi mengi yanayo athiri mambo yao wenyewe na mamo yaw engine.  Ngazi mbili zinahusika katika kufanya maamuzi:

Katika ngazi ya kwanza, raia wanahitajiwa kukusanya habari muhimu kwa kutumia nyenzo za maulizo (kuangalia, kueleza, kulinganisha, kutambulisha, n. k.).  Halafu wanahitajiwa kuamua ukweli wa habari hiyo ambayo wanatumia kama ushahidi wa kuunga mkono nafasi yao katika matatizo mchanganyiko ya kijamii. Kutoka shindano linalodai ukweli, raia anahitajiwa kuwamua anachokiamini.  Wanahitajiwa kutofautisha dai la uhakika thabiti toka yale yasio.  Hata hivyo, matatizo mantiki hutokea umakinifu wa fikra unapotumika (kwa mfano, ubinafsi, kufanya ulinganisho kimakosa, kusema vitu kila mtu atakipenda, kubishana kwa kuzunguka, n.k.) (Callahan, 1998).  Zaidi ya hayo, makosa ya kawaida yanafanywa wakati nakala rahisi (utaratibu wa uendeshaji wa kiwango, usemi wa zamani, kutumia mazingira yaleyale, etc) yanatumiwa kufanya maamuzi mchanganyiko.  (Callahan, 1998) .  Matatizo haya huja tunapojaribu kujiambia wenyewe ukweli kuhusu vitu tunavyofanya na maamuzi tunayofanya.  Raia anahitaji kuelewa matatizo haya na kujiandaa kuyakabili.

Katika ngazi ya pili, raia anahitajiwa kuamua jinsi ya kukabiliana na matatizo mchanganyiko ya kijamii: jinsi ya kufafanua matatizo, dsesturi gain zifuatwe, sheria gain za nchi zi saidiwe, mgombea gain achaguliwe kushika ofisi, hatua gain zichukuliwe kulingana na matakwa ya jamii (Engle & Ochoa, 1998, p. 61).  Kufanya nini, raia anatakiwa kufuata modeli ambayo inaweza kuendelea tunachokifikiri na kuamini.  Wanaweza kufanya haya kwa:

  • Kuzungumza kuhusu hali na wengine
  • Cheki kuona kuwa kama wana habari za kweli za kutosha na kama kuna upendeleo katika mafikirio yao
  • Cheki kuona kuwa kama wana habari za kweli za kutosha na kama kuna upendeleo katika mafikirio yao
  • Kutumia mihemuko kuonyesha umuhimu lakini sio kama ndio tabia pekee
  • Kutofautisha kati ya tatizo na jawabu linalowezekana (kutenganisha nyezo toka jawabu)
  • Kufikiria njia tofauti kuendelea na kuona ni hali gain itashawishi vipingamizi kwa kila jawabu linalowezekana
  • Kushirikiana kuchanganua njia mbalimbali za kuendelea
  • Kuamua njia zipi zinafaa na kitu gani kinachofuata kifanywe

Steiner (kama ilivyonukuria katika Lipset, 1995) ilishughulikia njia sahihi za kufanya maamuzi.  Alisisitiza kuwa katika jamii ya kidemokrasia watu wengi iwezekanavyo wanatakiwa kujihusisha katika kufanya maamuzi.  Ufanyaji maamuzi unatakiwa uwe wazi kwa watu ili watu wengi waweze kuhusishwa. Mazunguzo ya watu yanaweza ku remba hoja na kuangalia umakinifu wa mijadala.  Matengenezo ya maamuzi yanatakiwa kuwa ni zaidi ya mkusanyiko wa mawazo yaliyoandaliwa awali.  Mawazo yanatakiwa yakabiliwe na na kila mmoja katika tufe la umma. Na washiriki wote katika mjadala huu wa umma wanapaswa kusikiliza mijadala yaw engine kwa kikweli. Kwa kufanya maamuzi sahihi ya kidemokrasia, hapakiwi kundi hata moja lisihusishwe (Lipset, 1995, p. 340).    Hapana chombo kingine chochote kinachoweza kuhusisha kuliko mtandao ambayo ni njia madhari ya kuongoza mda na nafasi katika njia ya kufikiri pamoja na kutengeneza maana

Katika demokrasia fikira za pamoja na kutengeneza maana ina maana ya kuunda fikra za pamoja za matukio.  Katika kutengeneza maana na kufikiri pamoja, mazungumzo yana maana zaidi.  Madhumuni ya mazungumzo maana yake ni”kutafuta uelewa wa pamoja na amani” (Webster kama inavyonukuriwa katika Yankelovich, 1999, p. 14).  Nidhamu ya majifunzo ya kitimu inaanza na mazungumzo, na uwezo wa mwanatimu kusitisha sadiki na kuingia katika fikira zao za pamoja zenye uhakika” (Sege, 1990)

Njia za mazungumzo zina hatua nne zifuatavyo:

  1. Kuangalia “taswira kubwa.”  Wote tunataka kuwa sehemu ya kitu kimoja “kizuri na kikubwa.” Tuanhitajia kufikiri pamoja ili kufanya haya yote yatokee.  Tunahitaji kusikiliza kwa masikio yetu, akili zetu, na mioyo yetu, katika sehemu iliyo salama.  Tunahitaji kusitisha maamuzi yetu.
  2. Kupambana na ubishani usiyokwepeka.   Baadhi ya watu wametoa rai ya mwongozo katika hatua hii intakiwa kuingizwa katika njia ya mazungumzo kimwili, kiakili, ana kiroho na kuwa macho kuwa nini kina roho na maana; na kusema, an kusikiliza ukweli bila lawama au maamuzi (Arrien, 1998).
  3. Kufany uchunguzi wa kweli.  Katika hatua hii, unafanya tamko, toa deta, ulizia, taka shauri, sikiliza, kataa majaribu ya kutokujitoa.
  4. Chukua muda wa kutafakari kikweli kweli, uthabiti, na uelewa.  Katika hatua hii, fikra zako zaweza kufuata njia hii: (Tupo sawa kuliko mimi; Tunaweza kufanya chochote, lakini kumbuka, hatuweza kufanya kila kitu; kwa hiyo kitu gani inachotufaa kufanya?).

Hill (2000) alinena yafuatayo kuhusu matokeo ya mazungumzo:

Splitter na Sharp (1995) anaelezea maulizo ya kijamii kama ni kujiribu kushirikiana kwa kikundi na jitihada za kutafiti hoja za kimatatizo kuunda maana kwa undani na maamuzi ya uhalali.  Katika mkazo wake wa maamuzi, jamii ya utafiti ina toa moyo kwa mwanachama kuwa mtu wa machanganuo (analytical)  zaidi, matakari, umakinifu na unenaji; kutoa mawazo yao na sababu zao kwa uhakiki na matakio ya mafanikio mema; na  kuendelea kufanya maamuzi makini. (ukurasa. 53)

Elimu ya kugawana madaraka na uwezeshaji inalenga kuwapa wanafunzi wachanga uelewa, uwezo, na ahadi ya kujitambulisha na kutenda kutokana na matakwa yao (Wallerstein & Bernstein, 1988, uk. 381-382) kiini na lengo la  Freire ni kwamba elimu sii kitu kisichosaidia upande wowote na hufanyika  kati ya maisha ya watu.  Kutokana naye, lengo la elimu ninapaswa kuwa ni kumkomboa binaadamu ili wanafunzi wawe ni walengwa na watendaji katika maisha yao na katika jamii.  Land na Gilbert (kama ilivyonukuriwa katika Husein na Psotlethwaite, 1994, uk. 1980) anadai kuwa tofauti kubwa nne ni ushahidi katika fasihi ya uwezeshaji kupitia a) ushindani wa binafsi b) uraia hai, c) uelewa yakinifu, na d) uwezeshaji tofauti.

Kwa ujumla, uwezeshaji un maanisha kutoa uwzo, kuruhusu au kuwezesha. KAtika uwanja wa elimu, kuwezesha ni kutambua uzoefu wa maisha ambao umetokana na histori, lugha, na mambo ya asili. Ni kuwawezesha wale ambao walikuwa wamegandamizwa kiuchumi na kimila na walioshindwa kudai heshima katika jamii zao. Hii ina maana zaidi tunaongelea kuwa wanafunzi ndio katika kitovu cha majifunzo yao. 

Uwezeshaji ni nafasi na ni njia thabiti ya kushiriki katika kugawana mamlaka.' (Bastian, Frucher, Gittel, greer, & Haskin, kama ilivyo nukuriwa katika Simon, 1987, Uk. 374). Mafundisho ya uwezeshaji ni muhimu katika kutathmin na kuhalalisha semi na imani za wanafunzi. "Inatambua sauti za wanafunzi hata wanapotetea kutambuliwa kwa sauti na fikra zao. Fikra za kimila ambazo zitia nanga kwa mambo wanayoyaamini" (Bastian, et, al., kama inavyonukuriwa katika Simon, 1987, uk. 377)

Mwisho, uwezeshaji unaweza kuwaongoza wanfunzi katika kukua kiakili (Hill, 2000). 

Kukuwa kiakili kunakoleta utambuzi, uelewa, na uwezo wa kupambana na hali yenye utata, mchanganyiko, na isiyo na uhakika inayoweza kutoka, na kujitokeza haraka sana, katika mazingira yanayomruhusu mwanafunzi kushuhudia nguvu na fikra na hasa mabadiliko ya kiakili kwenye mazingira yanayowaunga mkono, na kuendelea kuwa katika mzunguko wa mazingira ya kuelewa yanajengwa katika fira na yana shuhurika na wengine katika rika lao, hawa ni pamoja na waalimu katika hali ya changanifu). Katika kuungwa mkono huku kunaweza kuleta mabadiliko ya haraka ya kimawazo, inayopelekea kuheshi na kuhusudu mawazo mapya wanayoyapata katka mazingira hayo, amabayo hujitokeza kwa vitendo.. (uk.61). 

Haya yote yanatokana na kuwa na mtu anayefaa kuwa katika mazingira yanayo mfaa kwa muda unaofaa- na ndio tu inaweza kutokana na mazingira yanayomuwezesha mtu hasa kuzingatia mazingira ya kiuchuku na hasa kwa kutumia tekinolojia.

Wazo lingine mugimu katika mfumo huu ni uwajibikaji: Wazo au ukweli wa kuwa mwajibikaji kwa kitu au kwa mtu/kwa kufanya kitu Fulani. Hii ina maana:

  • Kuwa na kaji au wajibu wa kufanya kitu Fulani au kumheshimu na kumtunza mtu
  • Fulani il uweze kulaumiwa kama kitu chocho hakitafanikiwa.
  • Kuwa na uwezo wa kuaminiwa, kupatikana, na kuelewa, (Oxford, 1996);
  • Kupatikana katika hali halali katika matukio ya halali ya utendaji Fulani;
  • Kuwa mtu anayewajibika kiroho kwa kila unachokifanya ama kinaweza kuwa cha kulaumiwa au kusifiwa, chochote kinachofanana na hayo.
  • Kuwajika kwa matendo kwa lolote unalotenda na uwezo wa kuyatawala hayo yote.

Kuwajibika katika matukio ya halali au kulalamikia katika hali zote (Hart, kama ilivyonukuriwakatika Glover, 1967, uk. 19). Uwajibikaji wa binafsi na uhusikaji wa kiraia na mengineyo ni ni mambo yanayokuwa na bahati katika demokrasia katika kugawana shughuli za pamoja kwa manufaa ya kikundi kizima pamoja na uhuru wa binafsi (Good, 1973). Mtu mmoja au ubinafsi una maanisha kuwa na uwezo wa kuelewa mahitaji ya wenzako katika kikundi na matatizo ya kikundi. Mtu anayewajibika hutaka mawazo ya kikundi kwa hali na uhalali wenye manufaa ya mahitaji ya kikundi. Mtu kama huyo anaweza kutoa hoja za mabadiliko kwa jinzi kikundi kinavyoppendelea. Uwajibikaji wa binafsi unatokana na nia ya mtu huyo na anavyoheshimu njia zate zinazofuata na kuamuliwa na kikundi kytatua matatizo kwa manufaa ya kikundi. Sio kujishusha kama uanweza kufuata na kufanya maamuzi yanayofanywa na kikundi kwa manufaa ya kikundi. Hii ni kushiriki kikamilifu kwa kutokana na hamu ya kufanikisha mambo yanapendelewa na kikundi." (Hollingshead, 1941, p. 43 - 44).

Kikundi kinaweza kuwa na uwajibikaji wa pamoja ambapo kila wajibu unamhusu mwana kikundi Kwa njia njingine kuwajibika katika kikundi kunaweza ukaletekeza tabia ya kujiundia uwajibika wa binafsi. Hii in a maana kuwa kama sisi sote tuna lengo la kitu kinachopendelewa na kikundi, basi njia nzuri ya kuweza kuwajibika katika kikundi na kila mmoja wetu ni kupeana au kugawana njajibu zinazoweza kuwa kwa manufaa ya kikundi. (Schmidtz & Goodin, 1998, p. 146 - 147)

Hollingshead (1941) alielezea wazo muhimu la kidemokrasia katika jamii.

Denokrasia si kikundi cha kisiasa, ila ni mahusiano katika jamii, ni utambuzi katika jamii ambao unapelekea kuendelea na kujiendeleza kwa mafanikio na malengo ya pamoja. Kugawana madaraka na uwajibikaji wa binafsi. Ni jinsi ya kuishi pamoja, kwa kuwa inakuwa kati ya watu na sio nje ya juu ya watu kwa sura za za kisiasa. Demokrasia ni umoja wa kijamii na sio ushindani. Ni jamii ambayo watu wanaishi kwa kushirikiana na wenzao na sio kushindana wenyewe kwa wenyewe. Ni jamii amabayo jamii inajitahidi kusaidiana na sio kunyoyana. (Holliganhead, 1941, p. 17 - 18)

Uwajibikaji wa kiraia, mahusiano ya jamii, uwajibikaji wa binafsi, mahusiano ya uanachama, kujitolea kiraia, kuaminiana kijamii, usalama wa jamii ni mambo mengine yota amabayo ni muhimu katika jamii ya kidomokrasia. (Putman, 1995).

Uwajibikaji wa binafsi una maana ya kuwa na matendo au shughuli za kujadili matendo, kama yanafanyika au la. Uwajibikaji wa binafsi una maana ya kuwa mtu m=binafsi ana uwezo wa kueleza shughuli kwa wale wanofanya kitu Fulani. "kwa kuonekana na uchaguzi wa kufanya mambo kwa makusudi ya kimatendo" Garfinkel, kama ilivyonukuriwa katika Shotter, 1967, uk. Vii). Tukio ni msaada wa fikirio, utendekaji, na uunganishaji wa mtiririko wa shughuli katika muoelekeo mmoja ambao unatambulika na wengi, kwa mfano, tukio ambalo linafahamika kw jinsi inavyoeleweka katika jamii (Shotter, 1984, Uk. 3).

Wazo la binafsi katika uelewa wa kikundi ni ni ujisikivu wa nguvu katika kikundi. Inavyoeleweka kutokana uelewa wa binafsi, kuwa mwanachama kunaonekana kutokana na mambo ya kikundi na wale wanaohusiana nao. Uanachama una maanisha kuwa mtu binafsi anaelewa yale yanayofanyiaka katika kikundi na ambayo yamefanikishwa kwa nguvu za wote wanaohusika katika kikundi hicho, pamoja na mambo ambayo wameamua kuyafanikisha wao wenyewe kama kikundi. Uanacham una maana kuwa na uwezo wa kuchangia katika mambo ya kikundi kwa manufaa ya kikundi kupitia uwajibikaji wa kiraia na kwa mchango wa wengine katika kikundi hicho. Uanachama una maanisha kuwa na wengine kwa nafsi zote kuwa na "usisi" nukuu ya udhamani ambayo inachukua nafasi ya "umimi"

Demokrasia ina nadharia ya kwamba unachama hutajirisha utu, kwa kuwa ina jitokeza katika hali ya kuongezeka kwa thamani, ikitambua kuwa mtu binafsi ana nafasi kubwa katika kuendeleza mambo yanayopendelewa na kikundi (Hollingshead, 1941, p. 41). Kujiamini kwa kijamii, na pia mambo mengine ya demokrasia, inrahisisha mawasiliano na kuhusika kwa manufaa ya kikundi kizima.

Marejeo

    The American Heritage Dictionary (2nd college ed.). (1982). Boston: Houghton, Mifflin.

    Arrien, A. (1998). Four-fold way [On-line]. Available: http://www.angelesarrien.com/four-fol.htm [2000, January, 13]

    Callahan, W. P. (1998). Common mistakes made when we make decisions [On-line]. Available: http://www.uni.edu/coe/admin/decisionmkg.html [1999, December]

    Engle, S. H., & Ochoa, A. S. (1988). Education for democratic citizenship: Decision making in the social studies. New York: Teachers College Press.

    Fisher, R., & Brown, S. (1988). Getting together – Building relationships as we negotiate. New York: Penguin Books.

    Good, C. V. (Ed.). (1973). Dictionary of education. New York: McGraw Hill.

    Hart, H. L. A. (1967). Varieties of responsibility. In J. Glover (Ed.), Responsibility (p. 19). New York: Humanities Press.

    Hill, L. (2000).  What does it take to change minds? Intellectual development of preservice teachers. Journal of Teacher Education, 51(1), 50-62.

    Hollingshead, A. D. (1941). Guidance in democratic living. New York: D. Appleton-Century.

    Husen, T., & Postlethwaite, T. N. (Eds.). (1994). The international encyclopedia of education (2nd ed.) (Vol. 2, pp. 1206-1207; Vol. 4, pp. 1980-1984). New York: Pergamon.

    Lipset, S. M. (Ed.). (1995). The encyclopedia of democracy (Vol. 2, p. 340). Washington, DC: Congressional Quarterly.

    Oxford-Advanced Learner’s Dictionary of Current English. (1996). Oxford: Oxford University Press.

    Putnam, R. D. (1995). Bowling alone: America’s declining social capital. Journal of Democracy, 6 (1), 65-78. Available: http://muse.jhu.edu/demo/journal_of_democracy/v006/putnam.html [2000, February]

    Schmidtz, D., & Goodin, R. E. (1998). Social welfare and individual responsibility. Cambridge: Cambridge University Press.

    Senge, P. M. (1990). The fifth discipline - The art & practice of the learning organization. New York: Currency Doubleday.

    Shotter, J. (1984). Social accountability and selfhood. New York: Basil Blackwell.

    Simon, R. I. (Ed.). (1987). Empowerment as a pedagogy of possibility. Language Arts, 64 (4), 374, 377.

    Wallerstein, N., & Bernstein, E. (1988, Winter). Empowerment education: Freire’s ideas adapted to health education. Health Education Quarterly, 15(4), 379-394.

    Webster's Ninth New Collegiate Dictionary. (1991). Springfield, MA: Merriam Webster.

    Yankelovich, D. (1999). The magic of dialogue: Transforming conflict into cooperation. New York: Simon & Schuster.