spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers
spacers home the model find a video Product spacer
spacer Help search Sitemap about
line

Ujuzi wa ndani wa Mwalimu Katika Masomo

 

     Ufupisho

Kwa kuwafundisha wanafunzi kutokana na kiwango cha leo, waalimu wanahitajika kuelewa somo kwa undani na kuwa warahisi kuwa saidia wanafunzi kuunda ramani za uelewa, kuhusianisha wazo moja na jingine, na kutatua mawazo potovu. Waalimu wanahitaji kuona ni namna gani wazo katika somo moja linafanana na wazo la katika somo jingine, na katika maisha yao ya kila siku. Hali ya uelewa huu hutoa msingi ya njia ya ufundishaji wa ujuzi wa somo ambao unawawezesha waalimu kuyafanya mawazo kupatikana kwa wengine (Shulma, 1987).

Shulman (1986) anatoa utanguizi kwa maneno njia za ufundishaji katika ujuzi wa somo (pedagogical content knowledge na na kuleta msisimko katika wimbi zima la maada ya kisomi inayozungumzia ujuzi katika somo na umuhimu wa ujuzi huo katika ufundishaji wenye mafanikio. Katika nadharia Shulman, waalimu wanahitaji kuwa na ujuzi wa aina mbili a) yaliomo, hasa ujuzi wa somo lenyewe kwa undani, na b) ujuzi wa maendeleo y amitaala. Ujuzi wa somo unaambatatisha kile ambacho Bruner (kama ilivyonukuriwa katika Shulman 1992) inavyokiita “Muundo wa ujuzi” Nadharia, kanuni, na mawazo katika somo fulani. Kilicho muhimu wa ujuzi katika somo kama inavyohusika na mfumo wa ufundishaji, inahusiana na jambo muhimu zaidi inayowasilisha somo na jinsi ambavyo mwanafunzi anajifunza wazo na somo fulani katika fani. “Kama waalimu wanaoanza kufundisha wanataka kufaulu, wanatakiwa wapambane vyema na mambo ja ujuzi wa ufundishaji (au ujuzi) na mbinu za ufundishaji kwa ujumla (au kanuni za ufundishaji kwa ujumla)” Grossman kama ilivyonukuriwa katika Ornstein, Thomas, & Lasley, 2000, p. 508).

Shulman 1986, 1987, 1992) aliunda model ya jinsi ya kutafakari ya ufundishaji ambao unaaambatanisha mzunguko wa kadhaa wa shughuli ambazo mwalimu anahitaji kufanikisha anapofundisha: kuelewa, kuleta mabadiliko, kufundisha, kutathmini, kutafakari, na kuleta elimu mpaya.

Kuelewa: Jambo la kwanza katika kufundisha ni kuelewa malengo, muundo wa somo, na mawazo ndani na nje ya somo. Waalimu wanahitaji kuelewa yale wanayofundisha na, inapowezakana, kuelewa kwa kwa njia njingi. Kuelewa sababu za kufundisha ni muhimu sana. Tunajihusisha katika kufundisha ili kufanikisha sababu kuu zifuatazo:

  • Kuwasaidia wanafunzi kufaidi masomo
  • Kuwawezesha wanafunzi kutumia na kufurahia uzoefu wao wa kujifunza
  • Kuendeleza uwajibikaji wa kujifunza wa wanafunzi ili wawe watu wanaojali
  • Kuwafundisha wanfunzi kuamini na kuwaheshimu wenzao, kutoa mchango wao katika jamii
  • Kuwapa wanafunzi nafasi ya kujifunza kutafiti na kugundua habari mpya
  • Kuwasaidia wanafunzi kuendeleza uelewa wa habari mpya kwa mapana zaidi
  • Kuwasaidia wanafunzi kuendeleza mbinu na thamani ili waweze kutumika kama watu huru na wenye nafuu katika jamii (Shulman, 1992)

Mabadiliko: La muhimu katika kutofautisha elimu ya msingi inakuwa kati ya njia panda ya somo ya njia za ufundishaji katika uwezo wa waalimu wa kufundisha na kuleta mabadiliko katika ujuzi wa somo na kubadilisha ujuzi huu katika wa ufundishaji na kuufanya uwe ni wenye nguvu zaidi na wenye kuelekea na uwezo mbalimbali wa wanfunzi na elimu yao ya awali. Kuelewa mawazo inahitajika kubadilishwa kwa kuchanganya au kuagizia mifumo ifuatayo:

  1. Maandalizi (kwa masomo fulali), ambayo inaunganisha mifumo kadhaa ya matafakari
  2. Mawasilisho ya mawazo katika mitindo ya kimethali mpya (ujuzi wa waalimu, inaunganisha jinzi inavyozungumzia kuhusu waalimu, sio tu kuwa na marejeo inayoelekeza kile waalimu wanachowajibika kufanya, inahusisha pia jinsi mwalimu anavyoweza kuwasilisha somo kwa kutumi lugha yenye mifano na mithali [Glatthorn, 1990]) 
  3. Uchaguzi wa ufundishaji kutoka mbinu na modeli nyingi za ufundishaji
  4. Kuiga masomo ya wanafunzi na shughuli zinazoelekea mitindo mbalimbali inayotumiwa na wanafunzi katika kujifunza
  5. Kufanikisha uigaji kwa wanafunzi fulani katika darasa
    Glatthorn (1990) anaelezea hii kuwa ni mfumo unalenga kulinganisha somo na tabia za wanfunzi. Mwalimu anatakiwa ajue vitu muhimu kuhusu uwezo wa wanfunzi, jinsia, lugha, mila, motisha, au elimu yao ya awali na mbinu ambazo zinaweza kuleta athari katika kuitikia somo wanapojifunza kwa jinzi zao tofauti na kwa kadri somo linavyowasilishwa.

Ufundishaji: pamoja na kuwa na matendo mbalimbali ya ufundishaji, uwezeshaji, uwasilishaji, kazi za vikundi, nidhamu, uchekeshaji, maulizo, na ugunduzi na ufundishaji wa kiutafiti.

Kutathmini: Waalimu wanahitajiwa kufikiria kuhusu kutoa majaribio na jinsi ya kutathmini kama njia ya kusaidia ufundishaji, sio kama mfumo tofauti wa ufundishaji. Mfumo wa kutathmini inaunganisha kukagua uelewa na kutokuelewa wakati wa miingiliano ya ufundishaji katika kila mwisho wa kipengele cha somo. Pia inahusisha utathmini wa utendaji na kuurekebisha utendaji huo katika mazingira tofauti.

Matafakari: Mfumo huu unahusisha, kurudia, kuunda, kutendesha, na kuchanganua kwa mbinu za ufundishaji kwa makini na kuweka maelezo hayo yaliyotafakariwa katika ushahidi uliojitokeza wakati wa mabadiliko ambayo yanahitajika kumfanya mwalimu kuwa mzuri. Hii ndio mwalimu hufanya anapoangalia nyuma wakati wa mafundisho na majifunzo yanayojitokeza, yanayotendeka, yanayoshikiaka katika matukio fulani, mihemuko, na mafanikio. Lucas (kama ilivyonukuriwa katika Ornstein na wenzake, 2000) anajadili kuwa matafakari ni sehemu muhimu ya maendelea ya kazi ya ufundishaji. Waalimu wote wnahitajiwa waifunze jinsi ya kuangalia matokeo na kutafunta njia za na sababu za kufaulu au kushindwa. Kupitia matafakari, waalimu wanalenga katika mahitaji, na kufikia kuelewa tabia zao za ufundishaji, kujisaidia wenyewe na wenzao kujiendeleza kama waalimu. Katka matendo na mazingira ya kimatafakari, waalimu hujifunza kusikilizzana wenyewe kwa wenyewe, ambavyo pia hutoa uelewa katika kazi zao wenyewe (Ornstein na wenzake, 2000). 

Uelewa mpya: Kupitia matendo ya ufundishaji ambayo “yamefikiriwa” na “kueleweka” mwalimu hufanikisha uelewa mpya wa makusudi ya kielimu, na somo linalofundishwa, na mfumo wenyewe wa ufundishaji (Brodkey, 1986).

Mwanafunzi ( ambao ni hadhara ya mwalimu) ni kipengele kingine muhimu kwa mwalimu kufikiria kutumia modeli ya ufundishaji. Mwalimu mwenye mbinu nyingi hutafiti kwanza kile mwanafunzi anachokielewa na anaamini anachokifundisha na jinzi ambavy wanafunzi wanaweza kufanikisha na kupata mawazo mapya. Ufundishaji unalingana na mahitaji ya wanafunzi pia uelewaji wa tofauti zinazoweza kutokana na mila na desturi, uzoefu wa kifamilia, akili ilivyokuzwa, na mifumo ya kujifunza. Mwalimu anahitaji kujenga misingi ya mbinu za ufundishaji (Grimmet & Mackinnon, 1992)

Kuwasaidia wanafunzi wote kujifunza, waalimu wanahitaji aina nyingi za ujuzi kuhusu kujifunza. Wanahitaji kufiri ina maana gani kujifunza vitu vingine vingi kwa sababu zingine na kuamua ni aina gani nyingine ya kujifunza iliyo muhimu katika mazingira tofauti. Waalimu wanhitaji kutambua udhaifu na uwezo tofauti wa wanafunzi na wanahitaji kuwa na ujuzi wa kufanya kazi na wanafunzi ambao wana mahitaji na shida katika kujifunza (k. m. v. walemavu). Walimu wanhitaji kujua kuhusu vifaa vya mitaala na tekinolojia kwa kuwaunganisha wanafunzi wao na mianzo ya habari na ujuzi ambao utawafanya wanafunzi waweze kuchunguza mawazo, kuulizia na kuunganisha habari, na kuunda na kutatua matatizo. Na waalimu wanahitaji kuelewa kuhusu kushirikiana-na jinsi ya kuunda ushirikiano kati ya wanafunzi ili ujifunzi wenye nguvu uweze kuonekana; na jinsi ya kushirikiana na waalimu wengine; na jinsi ya kufanya kazi na wazazi kujifunza zaidi kuhusu watoto wao na kuunga mkono unoaji wa uzoefu wao wa shuleni na nyumbani (Shulman, 1992).

Upataji wa huu ujuzi mchanganyiko na kuendeleza mazoezi amabayo ni tofauti na yale ambayo waalimu wenyewe waliyazoea wakati wakiwa wanafunzi, unahitaji waalimu wapewe nafasi ya kujiendeleza ambao utawapa nguvu za kutenda inavyotakiwa licha ya kusoma na kuongea tu kuhusu mbinu mpya za ufundishaji (Ball & Cohen, 1996). Waalimu hujifunza vizuri zaidi kwa kusoma, kwa kufanya na kutafakari, kwa kushirikiana na waalimu wengine, kwa kuwaangalia wanafunzi na kazi zao kwa ukaribu zaidi, na kushirisha wengine kile wanachokiona.

Aina hii ya kujifunza haiwezi ikaonekana katika madarasa ya chuoni ambayo yametarakishwa na mazoezo au madarasa yaliyotarakishwa na elimu hasa jinsi ya kutafsiri mazoezi. Mazingira mazuri ya kujifunza katika vyuo na mashule – inatoa nafasi kubwa sana ya utafiti na udadisi, kwa kujaribu na kutoa majaribio, kwa kuyaongelea na kutathmini matokeo ya kujifunza na kufundisha. Miungano ya nadharia na matendo (Miller & Silvermail, 1994) inajitokeza vizuri zaidi kwa maswali yanayojitokeza katika mazingira ya kweli ya wanafunzi na wakati kazi inaendelea na mahali ambapo utafiti na nidhamu ya kimaulizo yanapatikana.

Darling-Hammond (1994) alinena yafuatayo:

Mazingira mazingira mazuri ya ujifunzi huo unatokea. Zaidi ya shule 3000 ya elimu katika America zimeunda programu amabayo ni zaidi ya kupata shahada ya kwanza ya miaka minne, inatoa elimu na kozi za masomo stahili ambayo inaungana na majifunzo maalum katika mashule. Zingine ni programu ya miaka miwili kwa mahafali wa shahada ya pili au kazi zozote zinazojitokeza wakati wa mafunzo (uk. 6)

Zingine ni modeli ya miaka mitano kwa waalimu waandaliwa ambao wataingia katka ufundishaji wakati wakiwa katika shahada yao ya kwanza. Kwa vyovyote, mwaka wa tano unawaruhusu wanafunzi kulenga katu katika shughuli zinazo waandaa wao kuwa waalimu, kwa muda wa mazoezi usiopungua mwaka mmoja ambayo ni moja ya mahitaji yao wanapochukua kozi za kufundisha na kujifunza. Utafiti umegundua kuwa mahafali kwenye programu hizi ndefu wanakuwa wameridhika na maandalizi haya, na wenzao, na mkuu wa shule, na waalimu washiriki wanawaona wao kama ni waalimu walioandaliwa vizuri zaidi.

Wote waalimu wa chuo na shule wana panga na kufundisha programu hizi. Waalimu wanaoanza hupata mwanzo mzuri unaolingamna uzoefu ambao wanpokuwa wamewekwa katika timu na waalimu hawa na wenzao. Waalimu wakongwe huendeleza elimu yao wanpokuwa wakifanya kazi kama wasaidizi, waalimu wasaidizi, watafiti washiriki na viongozi wa waalimu. Kwa hiyo, shule hizi zinaweza zikaunda ungano kati ya nadharia na matendo, ambapo ikiunda ufanisi mkubwa wa kikazi kati ya waalimu na kuunda ujuzi ambao una utumi mkubwa sana kwa matendo na ujenzi wa nadharia unaoendelea (Darling-Hammond, 1994). 

Kama waalimu watachunguza madhara ya ufundishaji wao kwa wanfunzi na kama watasoma yale ambayo yamesemwa na wenzao, wanakuwa wanaelewa tofauti zao na kuelewa kinachofanya kazi na kwa sababu gani na katika mazingira gani. Majifunzo ya kujiuliza pia yawasaidia waalimu kuwa na uwezo wa kuitazama dunia katika mitazamo mingi na kutumia ujuzi huu kuwafikia na kuwa saidia wanafunzi kutoka tabaka nyingfi. 

Marejeo

            Ball,  D. L.,  &  Cohen,  D. K. (1996).  Reform by the book: What is--or might be--the role of curriculum materials in teacher learning and instructional reform?  Educational Researcher, 25(9),  6-8.

           Brodkey,  J.  J.  (1986).  Learning while teaching. Unpublished doctoral dissertation, Stanford University.

           Darling-Hammond, L.  (1994, September).  Will 21st-century schools really be different? The Education Digest, 60, 4-8.

            Glatthorn, A.  A.  (1990).  Supervisory leadership.  New York: Harper Collins.

            Grimmet,  P., &  MacKinnon,  A.  (1992).  Craft knowledge and the education of teachers.  In G. Grant (Ed.), Review of research in education 18, pp. 59-74  Washington, DC:  AERA.

            Miller,  L.,  &  Silvernail,  D.  L.  (1994).  Wells Junior High School: Evolution of a professional development school.  In L.  Darling-Hammond (Ed.), Professional development schools: Schools for developing a profession (pp.56-80).  New York: Teachers College Press.

            Ornstein,  A.  C., Thomas,  J.,  &  Lasley,  I.  (2000).  Strategies for effective teaching.   New York:  McGraw-Hill.

            Shulman,  L.  (1986).  Those who understand: Knowledge growth in teaching. Educational Researcher15 (2), 4-14.

            Shulman,  L.  (1987).  Knowledge and teaching: Foundations of the new reform.  Harvard Educational Review,   57 (1),  1-22.

            Shulman, L. (1992, September-October). Ways of seeing, ways of knowing, ways of teaching, ways of learning about teaching.  Journal of Curriculum Studies, 28,  393-396.